Na mwandishi wetu
Mechi za Ligi Kuu NBC za Azam FC dhidi ya Yanga ya Machi 17, mwaka huu na ile ya Simba itakayopangiwa tarehe baadaye, zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo Jumanne na meneja wa uwanja huo, Milinde Mahona akisema Azam walituma maombi ya kutumia uwanja huo na wamekubaliwa na muda utapangwa kati ya 2.30 na 3.00 usiku.
“Ni kweli mechi mbili za Azam dhidi ya Yanga na Simba zitachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na tutatolea ufafanuzi kwa nini tumeruhusu,” alisema Mahona.
Awali Serikali ilitangaza kufunga Uwanja wa Mkapa na wa Uhuru, Desemba mwaka jana mpaka pale ukarabati utakapomalizika Oktoba, mwaka huu lakini iliruhusu mechi za kimataifa za Ligi ya Mabingwa Afrika za Simba na Yanga kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Timu zilizoomba kutumia viwanja hivyo kama viwanja vyao vya nyumbani zimeelekezwa kutafuta viwanja vingine ambazo ni Simba, Yanga na KMC ambayo ilikuwa inatumia Uwanja wa Uhuru.
Soka Yanga, Simba kuikabili Azam Kwa Mkapa
Yanga, Simba kuikabili Azam Kwa Mkapa
Read also
