Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemkabidhi mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas mipira 1,000 kwa ajili ya kuigawa katika shule za msingi ili kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi kwenye shule hizo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mipira hiyo, Kanali Abbas amezitaka shule hizo kuitumia mipira hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na TFF ambayo ni kuibua vipaji vya wanafunzi mashuleni.
“Naomba kusisitiza kwenye halmashauri na wilaya waongeze jitihada za kuwajengea uwezo vijana hawa na vipaji vipo, kinachotakiwa ni kufanya mashindano kuanzia ngazi za chini lakini pia mipira hii itumike kwa malengo yaliyokusudiwa’’alisema Abbas.
Kiongozi huyo ameishukuru TFF na kusema watahakikisha wanafanya jitihada za lazima kuinua viwango vya mchezo wa mpira miguu mkoani humo ambapo sasa wanaenda kujenga uwezo kwa vijana wao kusajiliwa na timu kubwa nchini.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara, Athumani Kambi alisema katika siku za hivi karibuni wataandaa mashindano maalumu kwa ajili ya kutimiza lengo la TFF ambalo ni kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wadogo na rika la kati.
Soka TFF yamwaga mipira 1,000 Mtwara
TFF yamwaga mipira 1,000 Mtwara
Read also
