Na mwandishi wetu
Timu ya Simba imejikuta pagumu kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Tanzania Prisons katika mechi iliyopigwa Jumatano hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Simba ambayo imetoka kuweka rekodi ya kuvutia kwa kuichapa Jwaneng Galaxy mabao 6-0 na kufuzu moja kwa moja robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ilitarajiwa kupata ushindi dhidi ya Prisons lakini mambo yakawa tofauti.
Mabao yaliyoibeba Prisons katika mechi hiyo kila moja lilipatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili mfungaji akiwa ni Samson Mbangula wakati Simba walipata bao pekee la kufutia machozi katika dakika za lala salama mfungaji akiwa Fabrice Ngoma.
Prisons katika mechi hiyo ilipata pigo na kujikuta ikibaki na wachezaji 10 uwanjani baada ya Mussa Haji kupewa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kumalizika ingawa Simba hawakuweza kutumia upungufu huo wa Prisons kupata sare au ushindi.
Matokeo hayo ni kama vile yanaikwaza Simba katika mbio za kulisaka taji la ligi hiyo kwani timu hiyo inabaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36 katika mechi 16 ikiwa imetanguliwa na Yanga inayoshika usukani na Azam FC iliyo nafasi ya pili.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa Jumatano hii matokeo ni kama ifuatavyo…
Mashujaa 1-0 Kagera Sugar
Azam FC 1-1 Coastal Union
Dodoma Jiji 1-0 Tabora United
Soka Prisons yaikwaza Simba
Prisons yaikwaza Simba
Read also
