London, England
Vigogo wa Ligi Kuu England (EPL) timu za Man United na Liverpool zimepangwa kuumana katika hatua ya rfobo fainali ya Kombe la FA katika mechi nyingine itakayokuwa ngumu na yenye ushindani.
Mechi hiyo itakuwa ni mwanzo wa hatua nyingine kwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kusaka taji la pili baada ya kufanikiwa kubeba taji la Carabao ikiwabwaga vigogo wengine wa England, Chelsea.
Kwa kocha Erik Ten Hag wa Man United naye ataingia katika mechi hiyo akisaka heshima kwa kuibwaga Liverpool lakini pia taji hilo linawezakuwa kitu muhimu kwake hasa kutokana na mabadiliko makubwa yanayotarajiwa kufanywa na tajiri mpya wa klabu hiyo, bilionea Sir Jim Ratcliffe.
Ratiba ya FA imekuja baada ya timu hizo kusonga mbele katika mechi zao za raundi ya tano, Man United ikiibwaga Nottingham na Liverpool ikiiweka pagumu Southampton kwa kuichapa mabao 3-0.
Man United katika mechi hiyo ilihitaji bao pekee lililowekwa kimiani kwa kichwa na kiungo wake Casemiro na sasa timu hiyo inajiandaa kwa mpambano mgumu hapo Machi 16 dhidi ya Liverpool.
Mabingwa watetezi wa taji hilo, Man City wao wamepangwa kuumana na Newcastle wakati Chelsea waliofanikiwa kuwabwaga Leeds United wamepangwa kucheza na vinara wa Championship, Leicester.
Mechi za robo fainali ya FA ni kama ifuatavyo…
Wolverhampton v Coventry City
Man United v Liverpool
Chelsea v Leicester City
Man City v Newcastle
Kimataifa Robo fainali FA ni Klopp v Ten Hag
Robo fainali FA ni Klopp v Ten Hag
Read also