Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kudhihirisha ubabe katika soka la Tanzania kwa kuinyuka Polisi Tanzania mabao 5-0 katika mechi iliyopigwa Jumanne hii usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Ushindi huo mnono katika mechi ya Kombe la Shirikisho Azam (FA) licha ya kuendeleza ubabe wa Yanga, pia ilikuwa nafasi ya kipekee kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Joseph Guede kuanza kuzifumania nyavu.
Guede aliyesajiliwa hivi karibuni ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzitikisa nyavu za Polisi katika dakika ya 13 kabla Farid Mussa hajaongeza bao la pili katika dakika ya 33.
Guede alikamilisha bao lake la pili na la tatu kwa Yanga katika dakika ya 45 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Mabao mengine mawili ya Yanga yalifungwa na Clement Mzize dakika ya 82 na Shekhan Khamis kwa mkwaju wa penalti dakika ya 86.
Timu nyingine za Ligi Kuu NBC ambazo zimewahi kukumbana na kipigo cha mabao matano mbele ya Yanga ni pamoja na mahasimu wao Simba, KMC na JKT Tanzania.
Soka Yanga yaitandika Polisi 5-0
Yanga yaitandika Polisi 5-0
Read also
