Na mwandishi wetu
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelipongeza Kundi la Ramadhani Brothers (pichani) kwa kuandika historia ya kuwa Watanzania wa kwanza kushinda mashindano makubwa ya kusaka vipaji ya American Got Talents: Fantasy League (AGT).
Rais Samia ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) kwa kuandika: “Pongezi kwa vijana wetu, Fadhili na Ibrahim kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League.
“Safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine,”.
Kundi hilo linaloundwa na ndugu wawili, Fadhil Ramadhani na Ibrahim Job walitangazwa usiku wa kuamkia jana Jumanne kuwa washindi kwa umahiri katika sarakasi na kuondoka na kitita cha Sh milioni 637.
“Hatimaye safari yetu imefikia hapa, tuna furaha kuwa washindi wa AGT Fantasy League duniani, asante kwa mashabiki wote na washiriki wenzetu,” waliandika kwenye ukarasa wao wa Istagram wa Ramadhani Brothers baada ya ushindi huo.
Kocha wa Acrobatic na meneja wa Ramadhani Brothers katika mashindano hayo, Winston Ruddle alisema: “Napenda kuwapongeza Ramadhani Brothers kwa kushika nafasi ya tatu katika Das Super Talent Ujerumani, mmeweka historia kama Watanzania wa kwanza na Waafrika wa kwanza kuwahi kushika nafasi hiyo ya juu Ujerumani, ninyi ni mabingwa wa kweli najivunia ninyi watu kutoka Afrika,”.
Mbali na pongezi nyingine kutoka sehemu mmbalimbali kwa kundi hilo Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) pia limewapongeza wasanii hao kwa kuiwakilisha vyema Tanzania.
Sports Mix Rais Samia awapongeza Ramadhan Brothers
Rais Samia awapongeza Ramadhan Brothers
Related posts
Read also
