Na mwandishi wetu
Ligi ya Mabingwa wa mikoa itachezwa kuanzia Machi 8, mwaka huu katika vituo vinne vya Njombe, Pwani, Manyara, na Mwanza ambapo kila kituo kitakuwa na timu saba.
Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jumapili hii, inasema ligi hiyo itachezwa kwa mkondo mmoja.
Kundi A litakuwa mkoa wa Njombe ikiwa na timu mwenyeji ya Hausing FC, Tutes Hub (Ruvuma), Don Bosco (Iringa), Tukuyu Stars (Mbeya), Mkwajuni FC (Songwe), THB FC (Rukwa) na Polisi Katavi (Katavi).
Kundi B litakuwa mkoa wa Pwani likiwa na timu mwenyeji Kiduli FC, Black Six (Dar es Salaam), Red Angels (Lindi), Stand FC (Mtwara), Moro Kids (Morogoro), Gunners FC (Dodoma) na Singida Cluster (Singida)
Kundi C ambalo ni mkoa wa Manyara mwenyeji ni Reggae Boys, Arusha City (Arusha), Kawele FC (Kilimanjaro), Veteran Middle Age (Tanga), Mabao FC (Shinyanga), Maswa FC (Simiyu) na Eagle SC (Dar es Salaam).
Rock Solutions ambao ni wenyeji wa Kundi D katika mkoa wa Mwanza, kundi hilo litakuwa na timu za Bweri FC (Mara), Bukombe Combine (Geita), Leo Tena (Kagera), Mambali Ushirikiano (Tabora), Kandahari FC (Kigoma) na Friends Rangers (Dar es Salaam).
Taarifa hiyo pia imefafanua kuwa klabu shiriki zinapaswa kuripoti kituoni kuanzia Machi 5, mwaka huu zikiwa na wachezaji wasiopungua 18 na viongozi wasiopungua watano.
Soka Ligi ya Mabingwa kuanza Machi 8
Ligi ya Mabingwa kuanza Machi 8
Read also
