Paris, Ufaransa
Klabu ya PSG ya Ufaransa inatajwa kumsaka mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen ikiamini kuwa mshambuliaji huyo anafaa kuvaa viatu vya Kylian Mbappe ambaye anatajwa kuwa na mpango wa kuihama klabu hiyo.
Mbappe imedaiwa hivi karibuni kuwa ameshatamka kwamba ataondoka PSG baada ya msimu huu na ingawa haijawekwa wazi klabu atakayojiunga nayo, Real Madrid ndiyo ambayo imekuwa ikitajwa sana.
Kigogo mmoja wa PSG amewahi kunukuliwa akisema kwamba klabu hiyo inataka kumkabisha Mbappe ingawa wanatambua kwamba lolote linaweza kutokea hivyo kama ikitokea akaondoka, Osimhen ndiye mtu sahihi wa kuchukua nafasi yake.
Osimhen, 25, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria na ndiye mwanasoka bora wa Afrika ameonesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu katika klabu ya Napoli.
Umahiri wa mshambuliaji huyo pia umezivutia klabu kadhaa barani Ulaya lakini PSG inaonekana kuwa juu katika mbio hizo na haitoshangaza mchezaji huyo akihamia katika klabu hiyo ya jijini Paris.
Ukiacha Osimhen, mshambuliaji mwingine ambaye amekuwa akitajwa kuwindwa na PSG ni Marcus Rashford wa Man United ambaye msimu huu unaonekana kuwa mgumu katika timu hiyo na hivyo anaweza kuwa tayari kwa ushawishi wowote wa kusaka changamoto mpya kwingineko.
Kimataifa Osimhen kumrithi Mbappe PSG
Osimhen kumrithi Mbappe PSG
Read also
