Na mwandishi wetu
Kocha msaidizi wa Azam FC, Bruno Ferry amesema anaamini kikosi chake kitabeba ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu huu licha ya ushindani mkali uliopo hivi sasa.
Kocha huyo alisema hiyo ni kutokana na ubora wa timu waliyonayo na malengo ambayo wamejiwekea katika kila mechi zinazowakabili mbele yao.
“Nakubali ligi ni ngumu, timu nyingi zimejiandaa vizuri wakiwemo mabingwa watetezi Yanga na Simba pia lakini hivi ni vitu vya kawaida, ninachoamini mwisho wa msimu Azam atakuwa bingwa kutokana na ubora wa kikosi chetu na maandalizi tuliyonayo tangu mwanzo wa msimu,” alisema Fery.
Mshindi huyo wa tuzo za kocha bora wa mwezi Novemba na Desemba, alisema anajivunia kikosi chake ambacho kimesheheni nyota wengi wenye uwezo mkubwa ukilinganisha na timu nyingine.
Alisema pamoja na kuondolewa kileleni na Yanga, lakini watapambana na kushinda mechi zilizopo mbele yao kuhakikisha wanarejea kwenye nafasi hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutimiza lengo lao.
Azam ipo nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo ikikusanya pointi 32 na Ijumaa ya wiki hii itamaliza mechi za mzunguko wa kwanza kwa kucheza na Geita Gold wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Soka Kocha aipa Azam taji la ligi kuu
Kocha aipa Azam taji la ligi kuu
Read also