Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za Kilimanjaro International Marathon zitakazofanyika Moshi, Kilimanjaro Februari 25, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne na waandaaji wa mashindano hayo, Kilimanjaro Marathon Company Limited, Dk Ndumbaro amethibitisha kushiriki na anatarajiwa kuongozana na viongozi wengine wa ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro na wa kitaifa.
“Wakati wa hafla hiyo, Dk Ndumbaro anatarajiwa kuanzisha rasmi mbio za kilometa 42 na zile za kilometa 21 na yeye kushiriki mbio za kilometa 5 za Gee Soseji,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo pia imeeleza namba na vifaa kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo zinazoratibiwa na Executive Solutions Limited, vitatolewa katika viwanja vya MoCU, kuanzia Februari 22 hadi Februari 24, mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni.
Mashindano hayo ya riadha maarufu Kili Marathon yamekuwa yakifanyika kila mwaka na kuendelea kujipatia umaarufu yakivutia washiriki wa ndani na nje ya nchi.
Riadha Dk Ndumbaro mgeni rasmi Kili Marathon
Dk Ndumbaro mgeni rasmi Kili Marathon
Related posts
Read also
