Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, Bakari Shime ameita kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu mashindano ya Olimpiki dhidi ya Afrika kusini.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Februari 19 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kisha timu hizo zinatarajia kurudiana Februari 28, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kikosi hicho kinaingia kambini kesho Jumapili lakini watamkosa mshambuliaji, Aisha Masaka ambaye anakipiga BK Häcken ya Ligi Kuu ya Sweden ambaye anasumbuliwa na majeraha.
Masaka alikuwa na kiwango bora katika mchezo wa raundi ya pili ambapo alipachika mabao mawili dhidi ya Botswana.
Huu ni muendelezo wa Twiga Stars ambao raundi ya pili waliiondosha mashindanoni Botswana kwa jumla ya mabao 3-0 ikishinda ugenini 2-0 kisha kushinda bao 1-0 nyumbani.
Kikosi kilichoitwa na kutangazwa Ijumaa hii kinaundwa na walinda mlango Najat Abas (JKT Queens), Asha Mrisho (Amani Quens) na Husna Mtunda (Yanga Princess).
Mabeki: Julietha Singano (Juarez, Mexico), Anastazia Katunzi (JKT Queens), Christer Bahera (JKT Queens), Fatuma Issa (Simba Queens), Violeth Nicholaus (Simba Queens) na Happy Hezron (JKT Queens).
Viungo: Ester Mabanza (JKT Queens), Aquila Gasper (Fountain Gate Princess), Stumai Abdallah (JKT Queens), Enekia Kasonga (Eastern Flames, Saudi Arabia) , Joyce Lema (JKT Queens) , Janet Christopher (JKT Queens), Amina Bilal (JKT Queens) , Diana Lucas (Ame S.F.K, Uturuki), Hasnat Ubamba (Fountain Gate Princess) na Irene Kisisa (Yanga Princess).
Washambuliaji ni Opa Clement (Besiktas, Uturuki) , Aisha Juma (Simba Queens), Donisia Minja (JKT Queens), Winfrida Gerald (JKT Queens) na Jamila Rajab (JKT Queens).
Soka Shime awaita 24 Twiga Stars
Shime awaita 24 Twiga Stars
Read also
