Na mwandishi wetu
Simba Queens (pichani) na Yanga Princess leo Alhamisi wanashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu kwenye Ligi Kuu Wanawake mzunguko wa tisa.
Wekundu wa Msimbazi ambao watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Nyankumbu dhidi ya Geita Queens, wanashika nafasi ya pili kwa pointi 19 tofauti ya pointi mbili dhidi ya kinara JKT Queens.
Simba inashuka dimbani ikiwa imetoka kushinda mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate, inakutana na Geita ambayo imetoka kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Yanga.
Geita yenyewe inaburuza mkia ikiwa na pointi moja na isipokuwa makini huenda ikachezea mvua ya mabao.
Yanga nayo iliyo nafasi ya nne kwa pointi 15, itacheza Uwanja wa Nyamagana, Mwanza dhidi ya Alliance Girls iliyo nafasi ya tisa kwa pointi sita.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni vinara JKT Queens watakaorindima kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuyo, Dar es Salaam wakiikaribisha Ceasiaa Queens.
JKT ni miongoni mwa timu mbili ambazo hazijapoteza mchezo wowote mpaka sasa ikiwa imeshinda michezo yote saba hivyo wanatazamiwa kuendeleza ubabe dhidi ya Ceasiaa.
Pia, kutakuwa na mechi ya Baobab Queens dhidi ya Amani Queens, Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na Bunda Queens dhidi ya Fountain Gate kwenye Uwanja wa Karume, Mara.
Soka Simba Queens, Yanga Princess dimbani
Simba Queens, Yanga Princess dimbani
Read also
