London, England
Kiungo wa zamani wa Everton, Man United na timu ya taifa ya Ubelgiji, Marouane Fellaini ametangaza kustaafu soka akiwa na miaka 36.
Fellaini ambaye ameichezea timu ya taifa ya Ubelgiji jumla ya mechi 87 na kushiriki fainali mbili za Kombe la Dunia, mwaka 2019 alitangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa.
Jina la Fellaini lilianza kupata umaarufu katika Ligi Kuu England (EPL) mwaka 2008 alipojiunga na Everton akitokea Standard Liege ya Ubelgiji kabla ya kutua Man United mwaka 2013 na baadaye mwaka 2019 alijiunga na klabu ya Shandong Luneng ya China.
“Imekuwa ni safari ya kipekee, nashukuru kwa kucheza mchezo ambao nimekuwa nikiupenda kwa kiwango cha juu,” alisema Fellaini kupitia mitandao ya kijamii.
Fellaini alisema anajivunia kizichezea klabu alizozichezea pamoja na heshima ya kuichezea timu yake ya taifa kuanzia Michezo ya Olimpiki mwaka 2008, Euro 2016 na fainali za Kombe la Dunia 2014 na 2018.
Akiwa na Everton, Fellaini alicheza jumla ya mechi 141 za EPL na kuifungia mabao 25 wakati kwa Man United ana rekodi ya kuifungia mabao 22 katika mechi 177 za mashindano yote, akiiwezesha kubeba Kombe la FA mwaka 2016, Europa Ligi na EFL mwaka 2017.
Kimataifa Fellaini atangaza kustaafu soka
Fellaini atangaza kustaafu soka
Related posts
Read also
