Na mwandishi wetu
Timu ya Taifa ya Kikapu ya Tanzanite haitashiriki michuano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopangwa kufanyika nchini Rwanda mwezi huu.
Awali, michuano hiyo ilitarajiwa kufanyika kuanza Februari Mosi hadi 10, mwaka huu kabla ya kuahirishwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari, Mary Arthur, Tanzanite haitashiriki michuano hiyo baada ya kupewa taarifa ya kuahirishwa hivyo itaendelea na majukumu mengine.
“Shirikisho lilipokea mwaliko kutoka serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wa kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoshirikisha michezo mbalimbali kutoka nchi wanachama,” alisema na kuongeza:
“Lakini baadaye tulipokea taarifa za kuahirishwa kwa mashindano husika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa waandaaji.
“Tanzanite haitashiriki michuano hiyo na kuwaomba radhi viongozi na mashabiki, wadau na dawati zima la ufundi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.”
Nchi nyingine zilizoalikwa awali kwenye michuano hiyo ni Kenya, Uganda, Burundi, Sudan Kusini, DR Congo, Somalia na wenyeji Rwanda.
Kikapu Kikapu wajitoa kwenye mashindano
Kikapu wajitoa kwenye mashindano
Read also
