Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Adam Adam amesema beki pekee anayemsumbua kwenye Ligi Kuu NBC ni Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (pichani) wa Yanga.
Akizungumza na GreenSports, kinara huyo wa mabao msimu huu kwenye kikosi cha Mashujaa alisema beki huyo ni miongoni mwa mabeki wachache wenye uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake na kuipa mafanikio timu yake.
“Ukweli kwangu Bacca ndiye beki bora kwenye ligi ligi yetu, ana uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake, maana ameonesha hilo akiwa na timu yake ya Yanga lakini hata timu ya taifa kule kwenye fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast,” alisema Adam..
Alisema amekutana na mabeki wengi wenye majina makubwa nchini akiwemo mkongwe Kelvin Yondani, Bakari Mwamnyeto na Juma Nyosso lakini Bacca ameonesha utofauti mkubwa kutokana na uchezaji wake.
Mshambuliaji huyo amewashauri viongozi kutoa kipaumbele kwa wachezaji wazawa kama ilivyofanya Yanga kwa Bacca kwani kama wakituliza akili wanaweza kupata wachezaji wengi wenye vipaji kuliko kutumia pesa nyingi kwenda nje ya nchi.
Soka Adam Adam akiri Bacca msumbufu
Adam Adam akiri Bacca msumbufu
Read also
