Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya ndondi inatarajia kuondoka nchini Januari 31 kwenda Kigali, Rwanda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika kuanzia Februari Mosi hadi 10, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga amesema kuwa wanatarajia kupeleka mabindia 10; wa kike watano na wa kiume watano, viongozi wawili ambao ni makocha
Samuel Kapungu na Rogate Ulaya huku mwamuzi ni Mafuru Mafuru.
“Majina ya mabondia yatatangazwa hivi karibuni na kwa sasa wanaendelea na mazoezi katika kambi ya JKT Mgulani na Uwanja wa Ndani wa Taifa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo ambayo tunajipanga kufanya vizuri,” alisema Mashaga.
Alisema mashindano hayo yatawasaidia kwa maandalizi ya Michezo ya Afrika itakayofanyika nchini Ghana kuanzia Machi 8 hadi 23 mwaka huu, ambako pia kutakuwa na michezo mingine zaidi ya ndondi.
Ngumi Timu ya ngumi kuondoka nchini Jtano
Timu ya ngumi kuondoka nchini Jtano
Read also
