Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha, amesema lengo lake ni kufanya vizuri na kushinda mataji akiwa na Wekundu wa Msimbazi ndio maana wamerejea kambini mapema kuanza maandalizi yao.
Benchikha alisema hayo Jumamosi hii baada ya kikosi chake kurejea kwenye uwanja wa mazoezi na kuanza maandalizi ya michezo ijayo ya Ligi Kuu NBC.
Simba imerejea kambini wiki chache tangu wapoteze mchezo wa fainali wa Kombe la Mapinduzi walipokubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mlandege.
“Tumerudi kwenye uwanja wa mazoezi na haya ni mazoezi yetu ya kwanza tukiwa na wachezaji wapya ambao wameungana na timu kwenye dirisha dogo .
“Tuliingia kambini tumeanza mazoezi ya uwanjani juzi na kuanza programu yetu, wachezaji walioko kambini wapo kwenye hali nzuri, niko hapa kwa miezi sita sasa na nataka kushinda mataji nikiwa hapa, nina furaha kuwa Tanzania, niko tayari kuanza kazi yangu,” alisema Benchikha raia wa Algeria.
