Na mwandishi wetu
Klabu ya mpira wa kikapu ya Pazi imeahidi kufanya vizuri katika mashindano maalumu yanayoshirikisha klabu bora za ukanda wa Afrika Mashariki yanayoanza kesho Jumamosi nchini Rwanda.
Akizungumza na waandishi kabla ya kuelekea Rwanda, Rais wa Pazi, Mussa Mzenji alisema kwa maandalizi waliyofanya ana uhakika watashiriki kiushindani na kufanya vizuri.
“Tuna uhakika tutafanya vizuri, tumejipanga na kila wakati tumekuwa tukijitahidi kuhakikisha tunajenga mahusiano mazuri na klabu mbalimbali, tutaendeleza kiwango bora na hatimaye kuwavutia wawekezaji waje watusapoti,” alisema.
Katibu Mkuu, Haby Mayeye alisema mwaliko huo umekuja kutokana na mafanikio ya mwaka jana ambapo walishiriki mashindano ya kufuzu Klabu Bingwa Afrika na kujitahidi kuonesha kiwango kizuri.
Alisema watahakikisha wanawakilisha vyema ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ya msimu huu.
Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Nicholas Mihayo alisema Pazi ni mfano wa kuigwa kutokana na kiwango bora ilichokionesha msimu uliopita na kuchangia kupata mwaliko huo wa kimataifa akisema anaamini watapeperusha vyema bendera ya nchi.
Kikapu Pazi waahidi mambo mazuri Rwanda
Pazi waahidi mambo mazuri Rwanda
Read also
