Na mwandishi wetu
Timu ya Al Najmah leo Jumatano imemtambulisha mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Simon Msuva kuwa mchezaji mpya wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia.
Msuva ametambulishwa na timu hiyo baada ya tetesi lukuki za kuwaniwa na Yanga SC katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo lililofungwa hivi karibuni.
Tetesi za nyota huyo kujiunga na Yanga ziliibuka baada ya kuvunjiwa mkataba na JS Kabylie ya Algeria na kuwa mchezaji huru mpaka anakwenda kwenye michuano ya Afcon inayoendelea Ivory Coast.
Hii ni mara ya pili mshambuliaji huyo aliyeondoka Yanga msimu wa 2017-18, anarejea Saudi Arabia baada ya kuwahi kuitumikia Al Quadsiah ya Ligi Daraja la Kwanza pia.
Baada ya Najmah kumtambulisha Msuva kwenye ukurasa wao wa mtandao wa Instagram, mshambuliaji huyo alieleza kufurahia kujiunga na timu hiyo ambayo kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi 25 baada ya mechi 18.
Soka Msuva apata timu Saudi Arabia
Msuva apata timu Saudi Arabia
Read also
