Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya PSG, Kylian Mbappe inadaiwa amekubali kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania ambayo ilihushwa naye kwa muda mrefu.
Mbappe anatarajia kujiunga na timu hiyo baada ya msimu huu akiwa mchezaji huru kwani atakuwa amemaliza mkataba wake wa sasa na PSG.
Habari zaidi zilizoripotiwa na vyombo vya habari Ulaya, zinadai kwamba, Real Madrid wamekubali kumchukua mshambuliaji huyo kwa makubaliano yanayodaiwa kuwa ya pesa pungufu ya zile za makubaliano ya mwaka 2022.
Wiki iliyopita mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alinukuliwa akisema kwamba bado hajaamua atakwenda timu gani baada ya mkataba wake na Real Madrid kumalizika.
Uamuzi wa Mbappe umekuja wakati Liverpool ikiwa tayari imetangaza nia ya kumsajili mshambuliaji huyo baada ya kuwapo habari kwamba mshambuliaji wao tegemeo, Mohamed Salah alikuwa mbioni kujiunga na klabu moja ya Saudi Arabia hivyo Mbappe alionekana kuwa mbadala sahihi wa Salah.
Habari nyingine hata hivyo zinadai kwamba Mbappe pia anaweza kujiunga na Liverpool au klabu yoyote ya Ligi Kuu England kama mambo ya Real Madrid hayatakwenda vizuri.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amewahi kunukuliwa akisema kwamba kikosi chake kimetimia bila hata ya kuwa na Mbappe hivyo haitoshangaza mchezaji huyo akielekea England.
Kimataifa Mbappe akubali kwenda Real Madrid
Mbappe akubali kwenda Real Madrid
Read also
