Na mwandishi wetu
Kipa wa Yanga, Djigui Diarra ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba wa timu hiyo na kuwa nyota wa tatu kushinda tangu tuzo hizo zilipoanza kutolewa Oktoba, mwaka jana.
Diara ametwaa tuzo hiyo baada ya kujikusanyia kura nyingi kutoka kwa mashabiki na kuwashinda beki wa kati, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ na mlinzi wa kushoto, Nickson Kibabage ambao waliingia tatu bora.
Diarra raia wa Mali ameshinda tuzo hiyo pamoja na pesa taslimu Sh milioni 4, ambazo hutolewa na mdhamini wa tuzo hiyo, Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Mchezaji wa kwanza kushidna tuzo hiyo alikuwa kiungo mshambuliaji na kinara wa mabao wa Ligi Kuu NBC, Stephen Aziz Ki alipowashinda Dickson Job na Max Nzengeli.
Mwingine aliyeibuka kidedea na kunyakua tuzo hiyo ni Pacome Zouzoua aliyeshinda mwezi Novemba baada ya kuwabwaga kiungo Khalid Aucho na mshambuliaji Clement Mzize.
Soka Diarra atwaa tuzo ya mwezi Yanga
Diarra atwaa tuzo ya mwezi Yanga
Related posts
Read also