Na mwandishi wetu
Shirikishi la Riadha Tanzania (RT), limepongeza hotuba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kugusa sekta ya ya michezo hususani kutambua mchango mkubwa uliotolewa na wanariadha.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu RT, Jackson Ndaweka, hotuba ya Rais Samia, mbali ya kugusa sekta mbalimbali, hakuisahau michezo hususani riadha kwa kuchangia mafanikio na kuitangaza vema Tanzania kimataifa kwa mwaka 2023.
“Sisi kama Riadha Tanzania tumeguswa na hotuba ya mheshimiwa Rais, tumefarijika pale alipotambua mafanikio ya wanariadha wetu Magdalena Shauri na Alphonce Simbu,” alisema Ndaweka na kuongeza:
“Hii itachochea kujituma zaidi na kufanya vizuri kwa vijana wetu na sisi kama shirikisho tunaahidi kujituma na kujipanga zaidi kwa kushirikiana na Serikali hususan wizara yenye dhamana na michezo, wadhamini na wadau mbalimbali ili kuleta mafanikio makubwa zaidi katika medani ya Riadha.”
Katika hotuba yake juzi, Rais Samia akielezea mafanikio katika sekta ya michezo alisema: “Kwenye sekta ya michezo, pamoja na kuimarisha miundombinu ikiwamo ukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa, mwaka huu tumepata mafanikio mengi ya kujivunia ikiwemo timu ya Yanga kupata medali ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
“Pia binti wa kitanzania Magdalena Shauri kuwa mshindi wa tatu kwenye mbio za Berlin Marathon na mwanariadha Alphonce Simbu kuwa mshindi wa pili kwenye mbio za Shanghai Marathon.”
Riadha RT wampongeza Rais Samia
RT wampongeza Rais Samia
Read also
