Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuufungia Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na TFF ikifafanua kuwa uwanja huo ambao umekuwa ukitumiwa na timu za Simba na KMC kwa michezo ya Ligi Kuu NBC, umekosa miundombinu na haukidhi matakwa ya kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu.
“Kufuatia uamuzi huo, timu zote zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Simba na KMC zinazokutana kesho Jumamosi kwenye mchezo wa ligi, zitautumia Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi hiyo.
Pia timu nyingine zilizokuwa zikitumia uwanja huo na sasa zinalazimika kutafuta uwanja mwingine ni pamoja na Cosmopolitan, Pan Africans na Green Warriors zinazoshiriki Ligi ya Championship.
Soka TFF yaufungia Uwanja wa Uhuru
TFF yaufungia Uwanja wa Uhuru
Related posts
Read also
