Madrid, Hispania
Real Madrid inatajwa kuanza hesabu za kumsajili kwa mara ya pili beki wa Man United, Raphael Varane ili kuziba pengo la David Alaba ambaye kwa sasa ni majeruhi.
Taarifa ya chanzo kimoja cha habari iliyopatikana leo Alhamisi ilieleza kuwa Real Madrid ambayo imefuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya Alaba kuwa majeruhi na jina la Varane limeingia katika hesabu zao.
Varane aliyekuwa na timu ya Ufaransa iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, ambaye amewahi kuichezea Real Madrid kabla ya kuihama mwaka 2021 na kusajiliwa na Man United, zipo habari kwamba kwa sasa hafurahii mambo ndani ya klabu hiyo.
Mwenendo mzima wa Man United na mfumo wa kocha Ten Hag ni kati ya mambo ambayo yanatajwa kutomfurahisha Varane na hivyo anaweza kushawishika kurudi kwa mara nyingine katika jiji la Madrid.
Habari zaidi hata hivyo zinadai kwamba kocha Ten Hag haonekani kuwa tayari kumruhusu beki huyo ambaye mkataba wake unafikia ukomo mwakani aondoke kwa kuwa yumo katika mipango yake na timu hiyo.
Ten Hag pia hataki kiungo wake Mbrazil, Casemiro aondoke licha ya wachezaji hao wawili wote kudaiwa kwamba kuna timu zinawataka na huenda wakaondoka wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari.
Kimataifa Real Madrid yamtaka Varane
Real Madrid yamtaka Varane
Read also
