Na mwandishi wetu
Mchakato wa kumpata kocha mkuu mpya wa Ihefu FC atakayerithi mikoba ya Moses Basena (pichani) umefikia katika hatua nzuri na wanatarajia kumtambulisha kabla mzunguko wa kwanza haujamalizika.
Katibu Mkuu wa Ihefu, Zagalo Chalamila alisema kwa sasa wanakamilisha baadhi ya taratibu ili wasaini mkataba na kuanza kazi kama ambavyo wamekusudia.
“Ni kocha wa viwango ambaye tunaamini atabadili mwenendo wa timu yetu na kutufikisha kule ambako tumekusudia kwa hiyo kupafika msimu huu ambako ni kumaliza kwenye nafasi nne za juu,” alisema Chalamila.
Kiongozi huyo alisema kingine kinachofanya wamlete kocha mpya kabla ya mzunguko wa pili ni kutaka kumpa nafasi ya kutoa mapendekezo yake kwenye usajili wa dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii.
Alisema kocha aliyepita Basena alishatoa mapendekezo yake kuhusu usajili wa dirisha dogo lakini wangependa kusikia na mapendekezo ya kocha wao mpya sababu yeye ndiye atakayekinoa kikosi hicho na kutimiza malengo ambayo wamempa.
Ihefu ambayo tayari imefukuza makocha wawili kabla ya mzunguko wa kwanza kumalizika msimu huu, inashika nafasi ya 13 ikiwa na idadi kama hiyo ya pointi na mechi walizocheza msimu huu.
Soka Mchakato mrithi wa Basena wafika pazuri
Mchakato mrithi wa Basena wafika pazuri
Read also
