London, England
Arsenal inataka kufanya mabadiliko kidogo katika safu ya kiungo ikiwania kumsajili kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz katika dirisha dogo la Januari huku majaliwa ya Thomas Partey yakiwa njia panda.
Hii si mara ya kwanza Arsenal kumtaka Luiz, jaribio la kwanza lilikuwa Septemba mwaka jana ambapo ofa ya Pauni milioni 25 iliyowasilishwa na timu hiyo, Villa waliikataa kabla ya mchezaji huyo kusaini mkataba mpya na Villa unaofikia ukomo mwaka 2026.
Kiwango cha Luiz hasa msimu huu kimeendelea kuishawishi Arsenal kuendelea na mipango ya kumsajili ikiamini mchezaji huyo anaweza kuwa msaada mkubwa kwa timu hiiyo katika michuano inayoshiriki.
Luiz, nyota Mbrazili, hadi sasa amecheza mechi zote 13 za Ligi Kuu England akiiwakilisha vyema Villa ambayo inashika nafasi ya nne katika ligi hiyo baada ya Jumapili kuichapa Tottenham mabao 2-1.
Arsenal haionekani kukata tamaa katika mbio za kumsaka mchezaji huyo lakini kilichopo ni kwamba italazimika kuboresha ofa yake ili kuishawishi Villa imuachie katikati ya msimu hasa kutokana na mafanikio ambayo timu hiyo imeanza kuyaona.
Tatizo linaloikabili Arsenal ni ufinyu wa bajeti licha ya kuhitaji kwa hali na mali huduma ya Luiz na ili kufanikisha hilo huenda ikalazimika kumpiga bei Partey ambaye hadi sasa ameanza mechi tatu tu za msimu huu akiandamwa na matatizo ya misuli.
Kimataifa Luiz wa Villa atakiwa Arsenal
Luiz wa Villa atakiwa Arsenal
Read also
