Na mwandishi wetu
Simba imeanza na sare ya bao 1-1 mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Wenyeji Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 44 mfungaji akiwa ni Saido Ntibazonkiza ambaye alifunga bao hilo kwa mkwaju ya panelti baada ya beki mmoja wa Asec kuunawa katika eneo la hatari mpira uliopigwa na Kibu Denis.
Serge Pokou aliisawazishia Asec bao hilo katika dakika ya 77 akineemeka na ushirikiano kutoka kwa William Sankara.
Simba katika mechi hiyo ilifanya mabadiliko matano ikiwaingiza, Clatous Chama, John Bocco, Luis Miquissone na Moses Phiri kuchukua nafasi za Ntibazonkiza, Che Malone, Kibu na Jean Baleke, mabadiliko ambayo hata hivyo hayakuweza kuipa bao timu hiyo..
Wakati Simba iliyokuwa nyumbani ikiishia kugawana pointi na timu hiyo ya Ivory Coast, katika michuano hiyo hiyo, jana Ijumaa mambo hayakuwa mazuri kwa mahasimu wao Yanga waliokuwa ugenini Algeria dhidi ya CR Belouizdad baada ya kuchapwa mabao 3-0.
Kimataifa Simba, Asec zatoka sare
Simba, Asec zatoka sare
Read also
