Na mwandishi wetu
KLABU ya Simba jioni ya Ijumaa hii imeweka wazi na kumtambulisha kocha wao mkuu mpya, Abdelhak Benchikha (pichani).
Simba imemtangaza Benchikha baada ya mazungumzo ya zaidi ya wiki tatu ikiwemo mazungumzo juu ya kumlipa mshahara wake unaotajwa kufikia zaidi ya Sh milioni 35 kwa mwezi inayotokana na ubora wa kocha huyo.
Benchikha ana uzoefu wa soka la Afrika kwa zaidi ya miaka 20 akitwaa mataji lukuki ikiwemo Kombe la Shirikisho la Afrika alilonyakua msimu uliopita dhidi ya Yanga SC akiwa na USM Alger kabla ya kuichapa Al Ahly mwanzoni mwa msimu huu na kutwaa ndoo ya CAF Super Cup.
Kocha huyo raia wa Algeria ambaye aliitema USM Alger hivi karibuni na kuwa huru ametua Simba kurithi mikoba ya Mbrazili, Roberto Olivera ‘Robertinho’ aliyefutwa kazi hivi karibuni kutokana na kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Yanga.
Mbali na USM Alger, Benchikha pia amewahi kuzinoa MC Alger, CR Belouizdad, Raja Casablanca, RS Berkane, Club Africain na nyingine ikiwemo timu ya taifa ya Algeria.
Tangu kuondoka kwa Robertinho, Simba imekuwa ikihusishwa na mipango ya kuwaajiri makocha kadhaa akiwamo Radhi Jaidi wa Tunisia mipango ambayo ni dhahiri sasa haipo tena.
Kimataifa Benchikha ndiye kocha mpya Simba
Benchikha ndiye kocha mpya Simba
Read also
