Na mwandishi wetu
Tuzo za wanamichezo bora za Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) zitaanza kutolewa kila mwezi kuanzia Januari hadi Desemba mwakani ambapo kutafanyika sherehe ya kuzawadia wanamichezo bora wa mwaka mzima.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi imetokana na kikao cha kwanza cha Kamati ya Tuzo hizo kilichofanyika Dar es Salaam wiki iliyopita chini ya mwenyekiti wa kamati hiyo, Jemedari Said (pichani juu).
Awali, mfumo uliokuwa umependekezwa ilikuwa tuzo zianze Julai, mwaka huu hadi Juni, mwakani lakini kamati imekubaliana kuwa kwa vile tuzo hizo zinaangalia michezo yote na si mchezo mmoja basi iwe kuanzia mwakani.
“Kamati ya Tuzo inaomba ushirikiano kwa waandishi wa habari za michezo kufanikisha tuzo hizi, na hilo litafanikiwa kama watashiriki kwa kupata taarifa sahihi za kila mwezi kuhusu matukio ya michezo mbalimbali,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na Jemedari.
Pia imeelezwa kuwa Kamati ya Tuzo ina furaha na kuona fahari kutimiza moja ya ndoto zilizosababisha kuundwa kwa chama hicho, nayo ni ya kuonesha kwa vitendo kuthamini wanamichezo waliong’ara katika michezo mbalimbali na zaidi kuwapongeza wale wanaofanya vizuri.
Sports Mix Tuzo za Taswa kuanza Januari
Tuzo za Taswa kuanza Januari
Read also
