Riyadh, Saudi Arabia
Winga wa Man United ambaye ana mgogoro na kocha wake, Jadon Sancho ni kati ya wachezaji wanaowindwa na klabu za Saudi Arabia kwa ajili ya kusajiliwa wakati wa dirisha la Januari mwakani.
Sancho kwa sasa ana mgogoro na kocha wake Erik Ten Hag, mgogoro ambao inatajwa kuwa huenda ukawa sababu mojawapo ya mchezaji huyo kuondoka katika klabu hiyo.
Sancho mwenye umri wa miaka 23 hata hivyo haijaelezwa kama atakuwa tayari kwenda kucheza katika Ligi Kuu Saudi Arabia maarufu Saudi Pro Ligi kwa kile kinachoaminika kuwa ni uamuzi wa kujishusha hasa kwa kuwa umri wake bado mdogo.
Ten Hag na Sancho waliingia katika mgogoro baada ya kipigo cha mabao 3-1 mbele ya Arsenal ambapo kocha huyo alisema kwamba hakumpanga mchezaji huyo kwenye mechi hiyo kwa sababu ya kuzembea mazoezini kauli ambayo Sancho aliipinga hadharani na kujikuta akiingia katika ugomvi na kocha wake.
Sancho mbali na Saudi Arabia pia zipo klabu kadhaa barani Ulaya zinazodaiwa kumuwania, mojawapo ya klabu hizo inayotajwa ni Juventus ya Italia ambayo imeonesha nia ya kumsajili kwa mkopo.
Mbali na Sancho mchezaji mwingine ambaye anatajwa kutakiwa Saudi Arabia katika usajili wa dirisha dogo la Januari ni mshambuliaji wa Tottenham, Richarlison ambaye naye bado hajaonesha dalili zozote za kuwa tayari kwenda kucheza katika Saudi Pro Ligi.
Kimataifa Sancho awindwa Saudi Arabia
Sancho awindwa Saudi Arabia
Read also
