Riyadh, Saudi Arabia
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu za Barcelona na Man City, Yaya Toure (pichani) ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Saudi Arabia na atakuwa msaidizi wa Roberto Mancini.
Yaya aliwahi kuwa chini ya Mancini katika klabu ya Man City, amepewa jukumu hilo ikiwa ni miezi takriban mitatu imepita tangu Mancini apewe majukumu ya kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Nyota huyo wa zamani wa Barca, aliichezea Man City kwa miaka minane kuanzia mwaka 2010 na kuanza kazi ya ukocha ambapo amewahi kuwa kocha katika akademi ya klabu ya Tottenham Hotspur.
Yaya mwenye umri wa miaka 40 sasa, pia amewahi kufanya kazi ya ukocha katika klabu za Donetsk Olympic ya Ukraine na Grozny ya Urusi.
Wakati akicheza soka la ushindani, ameiwakilisha timu ya taifa ya Ivory Coast mara 101 na kuiwezesha kubeba Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 na kushinda mataji 18 katika klabu mbalimbali barani Ulaya katika nchi za Ugiriki, Hispania, England na China.
Saudi Arabia kwa sasa inapambana kuinua hadhi ya soka lake ikitajwa kuwa katika maandalizi makali ya fainali za Kombe la Dunia 2034 ambapo nchi hiyo inatajwa kuwa mwenyeji.
Kimataifa Yaya Toure kocha msaidizi Saudi Arabia
Yaya Toure kocha msaidizi Saudi Arabia
Read also
