London, England
Usajili wa wachezaji Samuel Eto’o na Willian katika klabu ya Chelsea mwaka 2013 ni kati ya matukio ya Ligi Kuu England yanayochunguzwa yakihusishwa na ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya fedha.
Julai mwaka huu, Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) ulitangaza kuitoza Chelsea faini ya Dola 10.65 milioni kwa kutoa taarifa za fedha zilizoonekana kuwa na utata zikihusisha biashara zilizofanyika kati ya mwaka 2012 hadi 2019.
Habari zaidi zilidai kwamba katika matumizi ya fedha yaliyofanyika katika kipindi hicho na ambayo yanafanyiwa uchunguzi yamo yale yaliyohusisha usajili wa winga Willian pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Samuel Eto’o.
Chelsea ilimsajili Willian huku habari zaidi zikidai kwamba mchezaji huyo alikuwa mbioni kusajiliwa na Tottenham kabla ya Chelsea kuvuruga mpango huo na siku chache baadaye alisajiliwa Eto’o ambaye pia alikuwa nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon.
Wachezaji wote hao waliosajiliwa mwaka 2013 walitokea klabu ya Anzhi Makhachkala ya nchini Urusi, wakati Willian kwa sasa anaichezea Fulham, Eto’o alistaafu soka miaka minne iliyopita na sasa ni rais wa chama cha soka nchini Cameroon.
Wakati matukio hayo yakitokea Chelsea ilikuwa ikimilikiwa na bilionea wa Urusi, Roman Abramovich ambaye aliinunua mwaka 2003 lakini mwaka jana alilazimika kuiuza baada ya Serikali ya Uingereza kudai kuwa alikuwa na ukaribu na rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye alikuwa akipigwa vita kwa kuivamia kijeshi Ukraine.
Kimataifa Usajili wa Eto’o Chelsea wachunguzwa
Usajili wa Eto’o Chelsea wachunguzwa
Read also
