Na mwandishi wetu
Siku mbili baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Baraza la Ushauri Simba SC, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameahidi kuhakikisha lengo mama la kuisaidia Simba kila eneo linatimia na kuipa mafanikio zaidi timu hiyo.
Kaburu ni miongoni ya wajumbe 20 walioteuliwa na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji au Mo chini ya mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Thomas Mihayo.
Akizungumza na GreenSports leo Jumanne, Kaburu alisema kwake ni faraja kubwa kuteuliwa kuwa miongoni mwa washauri kwani inaonesha ni jinsi gani wadau wamekuwa na imani naye hata baada ya kumaliza kuwahi kuiongoza klabu hiyo.
“Ni imani kubwa iliyooneshwa kwangu kwamba nilishawahi kuwa kiongozi na sasa nimepewa nafasi ya kutoa mawazo yangu kwa uongozi uliopo,” alisema Kaburu aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Simba na kuongeza:
“Lengo kubwa ni lengo mama la kuhakikisha Simba inazidi kwenda mbali na inafikia malengo madogo na makubwa, kikubwa Simba ni Nguvu Moja hivyo mashabiki, wanachama wote tuwe pamoja na wawekezaji, wadhamini na uongozi kuhakikisha Simba yetu inafikia pale tunapotarajia.”
Mbali na Kaburu, wajumbe wengine ni Hassan Dalali, Ismail Rage, Evans Aveva, Faroukh Baghoza, Swedi Nkwabi, Azim Dewji, Kassim Dewji, Musley Al-Ruweh, Mohamed Nassor, Mulamu Ng’ambi, Octavian Mshiu, Mohamed Janabi.
Wengine ni Hassan Kipusi, Gerald Yambi, Moses Kaluwa, Crescentius Magori, Juma Pinto, Mwina Kaduguda na Idd Kajuna.
Soka Kaburu ajipanga kuisaidia Simba
Kaburu ajipanga kuisaidia Simba
Related posts
Read also
