London, England
Hatimaye England imefuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 (Euro 24) baada ya kuichapa Italia mabao 3-1 katika mechi ambayo ubora wa kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham ulijidhihirisha kwa mara nyingine.
England ilikuwa ikihitaji pointi moja ili kufuzu ingawa Italia walitaka kuvuruga sherehe baada ya kuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 15 lililofungwa na nyota wa zamani wa West Ham, Gianluca Scamacca.
Juhudi za Bellingham hadi kuchezewa rafu na mwamuzi kutoa penalti dakika ya 32 kuliipa England bao la kusawazisha lililofungwa na Harry Kane kwa mkwaju wa penalti. Kane sasa anakuwa amefikisha mabao 60 na timu ya England.
Bellingham, 20, kwa mara nyingine alitengeneza bao la pili la England katika dakika ya 57 baada ya kumuunganishia pasi Marcus Rashford ambaye aliitumia vyema kuipatia England bao kabla Kane hajamalizia kwa bao la tatu dakika ya 77.
England kwa sasa inashika usukani Kundi C ikiwa na pointi 16 wakati Italia inashika nafasi ya tatu na itacheza mechi yake ya mwisho na Ukraine, mechi ambayo itaamua kama timu hiyo itashika nafasi ya pili na kufuzu au la.
Ushindi wa England dhidi ya Italia umedhihirisha kwa mara nyingine uwezo wa Bellingham ndani ya kikosi cha timu ya taifa baada ya kutamba katika klabu kwani alihusika na kujitoa katika kila hatua ya mechi hiyo hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Matokeo ya mechi za kufuzu Euro 2024…
England 3-1 Italia
Ireland Kask 0-1 Slovenia
San Marino 1-2 Denmark
Finland 1-2 Kazakhstan
Malta 1-3 Ukraine
Lithuania 2-2 Hungary
Serbia 3-1 Montenegro
Kimataifa England yafuzu Euro 24
England yafuzu Euro 24
Read also