Manchester, England
Manchester City inajipanga kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake, Erling Haaland lengo likiwa ni kuzima ushawishi wa klabu za Barcelona na Real Madrid zinazodaiwa kumtaka mshambuliaji huyo.
Kinara huyo wa mabao wa Ligi Kuu England (EPL), ndiye aliyetoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kubeba mataji matatu (treble) ya FA, EPL na Ligi ya Mabingwa Ulaya, anawindwa pia na klabu nyingine barani Ulaya.
Katika mkataba huo mpya, Man City wanadaiwa kuondoa baadhi ya vipengele kwenye mkataba wa awali lengo ni kuondoa uwezekano wowote kwa mchezaji huyo kuhamia timu nyingine hususan Real Madrid au Barcelona ambazo ndizo zinazotajwa zaidi.
Awali zilikuwapo habari kwamba katika mkataba wa Haaland kulikuwa na kipengele ambacho kinampa nafasi mchezaji huyo kujiunga na Real Madrid jambo ambalo lilikanushwa na kocha wa Man City, Pep Guardiola.
Real Madrid inadaiwa bado wana imani ya kuwa na ushawishi wa kumpata mshambuliaji huyo aliyejiunga na Man City akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani
Kimataifa Haaland kupewa mkataba mpya Man City
Haaland kupewa mkataba mpya Man City
Read also