Newcastle, England
Newcastle imerudi kwa kishindo St James Park ikiichapa PSG mabao 4-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi ambayo ni ya kwanza kwa timu hiyo kucheza nyumbani tangu mwaka 2003 iliposhiriki kwa mara ya mwisho mashindano hayo.
Ushindi wa Newcastle mbali na kufurahiwa na mashabiki lakini unaacha maswali PSG kuhusu shauku ya timu hiyo kutamba Ulaya msimu huu baada ya kushindwa kuonesha makali katika misimu ya hivi karibuni licha ya kusheheni wachezaji mastaa akiwamo Lionel Messi.
PSG ikiwa na kinara wake wa mabao Kylian Mbappe ilijikuta katika wakati mgumu ugenini kwa kupata matokeo yanayoacha maswali kuhusu mwelekeo wa timu hiyo katika ligi hiyo kubwa barani Ulaya.
Ikishingiliwa na mashabiki wake waliolipamba dimba la St James kwa jezi za rangi nyeusi na nyeupe, Newcastle waliandika bao la kwanza dakika ya 17 mfungaji akiwa ni Miguel Almiron.
Kipa wa PSG, Gianluigi Donnarumma alishuhudia nyavu zake zikitikiswa tena mara tatu kwa mabao ya Burn dakika ya 39 na Longstaff dakika ya 50 na Schar dakika ya 90 wakati bao pekee la PSG lilifungwa na Lucas Hernandez dakika ya 56.
Matokeo hayo ya jana Jumatano yanaifanya Newcastle kufikisha pointi nne baada ya kutoka sare na AC Milan na sasa inashika usukani katika Kundi F.
“Tumefurahishwa na matokeo haya, zilikuwa ni juhudi za kipekee kutoka kwa wachezaji, hii ilikuwa mechi tofauti, ilikuwa ni kama paka na panya, tulikuwa tukijaribu kuwakimbiza nao walikuwa wakipambana kucheza kwenye eneo letu,” alisema kocha wa Newcastle, Eddie Howe.
Matokeo ya mechi za Jumatano za Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Celtic 1-2 Lazio
Newcastle 4-1 PSG
RB Leipzig 1-3 Man City
FC Porto 0-1 Barcelona
Atl Madrid 3-2 Feyenoord
Royal Antwerp 2-3 Shakhtar Donetsk
B Dortmund 0-0 AC Milan
Red Star Belgrade 2-2 Young Boys