Na mwandishi wetu
Siku mbili baada ya Tanzania, Uganda na Kenya kutangazwa kuwa waandaaji wa fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2027 (Afcon), imewekwa wazi kuwa kwa Tanzania vitatumika viwanja vitatu katika michuano hiyo.
Akizungumza leo Ijumaa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Ally Mayay alisema viwanja vitakavyotumika ni Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Uwanja wa Amaan wa Zanzibar na Uwanja wa The Hexagon uliopo Arusha unaotarajia kuanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka 2024.
“Viwanja vya mashindano ni vinane kwa nchi hizi tatu, Tanzania tulichagua ule wa Benjamin Mkapa, Uwanja wa Amaan Zanzibar na uwanja mpya wa Arusha. Ni uwanja wa kisasa ambao unajengwa nje ya mji, Kata ya Olmoti na utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 30,000 waliokaa,” alisema Mayay.
Uwanja wa Mkapa ndio mkubwa zaidi Tanzania na Afrika Mashariki wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000, huku Uwanja wa Amaan ukiwa na uwezo wa kuingiza kuanzia mashabiki 15,000.
Tanzania, Uganda na Kenya ambazo zimeita umoja huo Pamoja Bid zilishinda kwenye kinyang’anyiro hicho juzi kwa kuzibwaga nchi za Misri, Senegal na Botswana wakati Algeria ilijitoa kwenye ushindani huo dakika za mwisho.
Soka Tanzania yataja viwanja Afcon 2027
Tanzania yataja viwanja Afcon 2027
Read also
