Manchester, England
Winga wa Man United, Antony amerudi England akitokea Brazil na amekubali kukutana na polisi wa Manchester ili kujibu maswali kuhusu tuhuma za udhalilishaji zilizowasilishwa dhidi yake.
Inadaiwa kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa, amekubali kuwakabidhi polisi wa Manchester simu yake ili kuwasaidia katika uchunguzi wanaoufanya dhidi yake.
Mwanadada, Gabriela Cavallin ambaye ni rafiki wa zamani wa kike wa Antony alinukuliwa na chanzo kimoja cha habari akiwasilisha tuhuma za kufanyiwa udhalilishaji na mchezaji huyo.
Tuhuma nyingine za udhalilishaji dhidi ya Antony ziliwasilishwa na wasichana wengine wawili, Rayssa de Freitas na Lana ingawa mchezaji huyo amekana tuhuma zote hizo.
Wakati yote hayo yakiendelea, klabu ya Man United, imetangaza kuzipa uzito unaostahili tuhuma hizo na wamempa Antony likizo ili kukabiliana na tuhuma hizo ingawa atakuwa akilipwa mshahara wake kama kawaida.
Antony alikuwa akiwajibika kwenye timu yake ya taifa ya Brazil wakati tuhuma hizo zilipotolewa na kujikuta akiondolewa katika kikosi cha timu hiyo mara tu baada ya kuibuka kwa tuhuma hizo kwa mara ya kwanza Septemba 4 mwaka huu.
Mmoja wa wasichana hao, Cavallin katika madai yake alidai kwamba Antony aliwahi kumpiga kichwa wakiwa katika chumba cha hoteli moja mjini Manchester na kumchana kichwani hadi kupatiwa matibabu na daktari.
Msichana huyo pia alidai kuumizwa kifuani baada ya kupigwa ngumi na Antony wakati Lana ambaye ni mtumishi wa benki alidai kusukumwa na mchezaji huyo hadi kujigonga ukutani, tuhuma ambazo pia Antony amezikana.
Kimataifa Antony ajisalimisha polisi Manchester
Antony ajisalimisha polisi Manchester
Read also
