London, England
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspur, Daniel Levy amesema katika mkataba wa mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane kuna kipengele kinachowapa nafasi wao kumsajili kwa mara nyingine.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Levy ametoa kauli hiyo ambayo haikufahamika kwa wengi hapo kabla ingawa hakusema moja kwa moja kama wana nia ya kukitumia kifungu hicho kumrudisha katika klabu hiyo mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya England.
Kane, 30, aliihama Tottenham mwanzoni mwa msimu huu akiacha rekodi ya kuwa mfungaji bora wa wakati wote katika historia ya timu hiyo na kujiunga Bayern Munich ambapo pia ameanza kutema cheche kwa kupachika mabao.
Uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Bayern ulikutana na vikwazo vya hapa na pale, sababu kubwa ikiwa ni Spurs kusita kumuachia mshambuliaji huyo ambaye pia alikuwa akiwindwa na klabu za Man United na Real Madrid.
Real Madrid ilishatangaza dau la Pauni 60 milioni lakini Kane ambaye pia alikuwa akiwindwa na PSG tangu awali alisema kwamba angependa zaidi kujiunga na Bayern.
Kwa upande wa Man United ilikuwa ikivizia kumsajili mshambuliaji huyo mara baada ya kumaliza mkataba wake na Tottenham na hivyo kumpata akiwa mchezaji huru.
Kimataifa Kane kurudishwa Spurs?
Kane kurudishwa Spurs?
Read also
