Manchester, England
Klabu ya Barcelona ya Hispania imejitosa ikitaka kumsajili mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland ikiamini kwamba inaweza kumpata kwa ada ya Pauni 150 milioni.
Chanzo kimoja cha habari kimeripoti kuwa Barca inapiga hesabu za kumpata mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwaka 2025 wakiamini ataweza kupatikana kwa thamani hiyo.
Barca hata hivyo ni lazima ijiandae kwa mchuano mkali kama kweli ina nia ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye pia amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na mahasimu wao wa Hispania, Real Madrid.
Real Madrid wameanza muda mrefu mbio za kumsaka Haaland hadi kuibuka habari kwamba klabu hiyo ilikuwa na makubalino maalum ambayo yangemfanya mchezaji huyo baadaye ahamia Real Madrid jambo ambalo hata hivyo kocha wa Man City, Pep Guardiola alilikanusha.
Kwa upande wa Barca, chanzo hicho hakijafafanua kwa undani nini hasa kimeifanya klabu hiyo kujiaminisha kwamba ina ubavu wa kumsajili mshambuliaji huyo ambaye mafanikio yake ya msimu uliopita wa 2022-23 yanatosha kutoa ushawishi kwa klabu yoyote duniani kuitaka saini yake.
Katika msimu huo Haaland alifunga jumla ya mabao 52 katika mechi 53 za michuano mbalimbali na kuiwezesha kwa kiasi kikubwa Man City kuweka rekodi mpya kwa kubeba kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo mataji matatu ya Ligi Kuu England, FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kimataifa Barca yajitosa, yamtaka Haaland
Barca yajitosa, yamtaka Haaland
Read also