New York, Marekani
Staa wa mchezo wa tenisi, Serena Williams sasa ni mama wa watoto wawili baada ya kujifungua mtoto wake wa pili ambaye pia ni wa kike kama wa kwanza na tayari amempa jina la Adira River Ohanian.
Taarifa ya Serena kupata mtoto iliwekwa juzi Jumanne kwenye mitando ya kijamii na mumewe, Alexis Ohanian ambaye alielezea furaha aliyokuwa nayo kwa mtoto huyo kuzaliwa akiwa mwenye afya pamoja na mkewe kujifungua akiwa mwenye afya.
“Nina furaha kuarifu kuwa nyumba yetu imejaa upendo, ni furaha, mtoto mpya wa kike mwenye afya na mama mwenye afya, Serena kwa mara nyingine umenipa zawadi isiyo na mfano, shukrani kwa madaktari wote,” alisema Alexis.
Kwa mara ya kwanza Serena alitangaza kuwa mjamzito mwenye Mei mwaka huu alipohudhuria hafla moja ya jioni akiwa na mumewe. Mtoto wa kwanza wa Serena na Alexis aitwaye Olympia sasa ana miaka mitano.
Serena mwenye umri wa miaka 41 sasa na ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa namba moja duniani katika mchezo tenisi, anatarajia kustaafu moja kwa moja mchezo huo hivi karibuni ingawa kumekuwa na mashaka kama atafanya hivyo licha ya kuahidi mara kadhaa.
Sports Mix Serena Williams apata mtoto wa pili
Serena Williams apata mtoto wa pili
Read also