Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeingia makubaliano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambna na Rushwa (Takukuru) kwa kuwa na kampeni ya kutoa elimu yenye lengo la kulinda hadhi ya mpira wa miguu nchini.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi na Mkurugenzi wa Sheria, Masoko na Habari wa TFF, Boniface Wambura (pichani) wakati wa kutambulisha kampeni ya ‘Kataa upangaji matokeo, linda hadhi ya mpira wa miguu’.
“Timu hii imeundwa kwa sababu TFF imekaa na kuona changamoto kwenye eneo hilo na kampeni itakavyokuwa inaendelea kwa kutoa elimu watu wajue ni jinsi gani ya kutoa taarifa.
“Ni kampeni ambayo tunafanya kuhakikisha elimu inawafikia watu ili mchezo uendelee kuwa wa kiungwana, na rasmi Jumamosi kutakuwa na bonanza ambalo lengo lake ni kutoa elimu juu ya kampeni hii,” aliongeza Wambura.
Bonanza hilo maalum litafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam Jumapili hii likiwa na timu sita ambazo ni TFF, Takukuru, Azam Media, Online Media, NBC Bank na Galacticos.
Pia alisema kwa kushirikiana na Takukuru haimanishi kuwa kanuni za mpira wa miguu hazifuatwi bali itasaidia kujua mazingira ya rushwa yanakuwaje na wanaposhirikiana watakuwa wanaelewa ni kitu gani kinaendelea kwa matukio ambayo wamepeleka Takukuru.
Naye Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa Takukuru, Joseph Mwaiswelo, alisema kila taasisi inatakiwa kushiriki katika kupambana na rushwa, ndio maana wameamua kushirikiana na TFF ili kuupa mpira hadhi yake inayotakiwa.
Soka TFF yawaita Takukuru kwenye soka
TFF yawaita Takukuru kwenye soka
Read also
