Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema wanaweza kuifunga timu yoyote kwani wana kikosi kizuri cha vijana wenye uzoefu kwa ajili ya kupambana kwenye Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Geita inatarajia kuondoka Jumapili hii kuelekea Mbarali, mkoani Mbeya kuifuata Ihefu kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kufungua pazi la ligi hiyo msimu 2023/2024 utakaochezwa Uwanja wa Highland Estate, Agosti 15, mwaka huu.
Akizungumzia maandalizi ya timu hiyo, Morocco alisema wamefurahia kambi ya maandalizi waliyoweka Morogoro kwani ilikuwa nzuri, wamepata muda wa kutosha kujiweka imara na sasa wako tayari kuanza harakati za kulipigania taji la ligi.
“Nimefurahia kambi yetu ya Morogoro. Wachezaji wako na afya njema na naamini wako vizuri kiakili na kimwili kuelekea katika mchezo wetu ujao dhidi ya Ihefu, naamini kwa kile nilichowaelekeza tutaanza vizuri Jumanne kwa kushinda bila kujali kuwa tunaanza ugenini,” alisema.
Morocco alisema kama ambavyo wengine wamesajili wachezaji wazuri hata wao pia wana kikosi kizuri kitakachowafikisha kwenye malengo waliyojiwekea.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Geita, Samwel Dida, jumla ya wachezaji 27 wataelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo na wengine watarudi Geita kujiandaa na mchezo ujao.
Soka ‘Tuna uwezo kuifunga timu yoyote’
‘Tuna uwezo kuifunga timu yoyote’
Read also