London, England
Liverpool huenda ikamkosa kiungo wa Brighton, Moises Caicedo (pichani) ambaye zipo habari kwamba Chelsea imempandia dau ikiwa tayari kutoa Pauni 115 milioni na haitoshangaza kiungo huyo akiachana na Liverpool.
Hivi karibuni, Liverpool ilitangaza kukubali kumsajili kiungo huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Ecuador kwa ada ya Pauni 111 milioni, hiyo ni baada ya awali Chelsea kutangaza kumtaka mchezaji huyo.
Uamuzi wa Chelsea kuongeza nguvu na kumpandia dau kiungo huyo utaiweka Liverpool pagumu baada ya kuamini kuwa Caicedo angesaidia kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo baada ya kuondoka kwa
Jordan Henderson na Fabinho waliotimkia Saudi Arabia.
Habari za ndani zinadai kwamba makubaliano ya awali baina ya Chelsea na Caicedo ni kwa mchezaji huyo kusaini mkataba utakaofikia mwisho Juni, 2031, ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Liverpool pia huenda ikazidiwa ujanja na Chelsea katika kuisaka saini ya kiungo wa Ubelgiji, Romeo Lavia ambaye kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari anatarajia kuihama Southampton na kutua Chelsea kwa ada ya Pauni 55 milioni.
Liverpool mbali na Caicedo pia ilionesha nia ya kumtaka Romeo ilipokwama kumsajili kiungo Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kujiunga na Real Madrid.
Mabosi wa Chelsea na Liverpool huenda wakakutana Stamford Bridge wakati timu zao zitakapoumana leo Jumapili katika mechi zao za kwanza za Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023-24.
Huenda usajili wa Caicedo na Romeo ukawaweka katika wakati mgumu mabosi hao ambao wote watakaa jukwaa kuu katika viti vinavyokaliwa na watu maalum.
Kimataifa Liverpool yapigwa bao, Caicedo aelekea Chelsea
Liverpool yapigwa bao, Caicedo aelekea Chelsea
Read also
