Na mwandishi wetu, Tanga
Benki ya NBC imetangaza kuongeza mkataba wa udhamini kwenye Ligi Kuu NBC kwa muda wa miaka mitano kuanzia msimu huu wa 2023-24 wenye thamani ya jumla ya Shilingi bilioni 32.56.
Mkataba huo ambao sasa utakuwa ukidhamini ligi tatu yaani Ligi Kuu NBC, Ligi ya Championship na Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 baada ya ule wa awali wa miaka mitatu uliokuwa na thamani ya Sh bilioni 2.5.
Mkataba huo umesainiwa leo Ijumaa kati ya NBC na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jijini Tanga ambako michuano mipya ya Ngao ya Jamii inaendelea.
Baada ya makubaliano yaliyosainiwa na Rais wa TFF, Wallace Karia na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, imetambulishwa rasmi kuwa Ligi ya Championship sasa itafahamika kwa jina la NBC Championship na Ligi ya Vijana U20 itaitwa NBC Youth League.
Sabi alisema kuwa wameendelea na udhamini huo kutokana na kupata baadhi ya faida ikiwemo uwezeshwaji wa ajira za moja kwa moja 7,000, ukuaji wa chapa ya benki ya NBC, ujumuishaji na uwezeshaji wa kifedha pamoja na kuchangia pato la taifa na kuchagiza shughuli za utalii.
Soka TFF, NBC wasaini mkataba wa bilioni 32
TFF, NBC wasaini mkataba wa bilioni 32
Read also
