Texas, Marekani
Barcelona imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu iliyopigwa Jumapili hii mjini Texas kwenye Uwanja wa AT&T.
Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Ousmane Dembele aliyefunga la kwanza yakifuatiwa na mabao mengine mawili ya Fermin Lopez na Ferran Torres.
Akizungumzia matokeo hayo hata hivyo kocha wa Barca, Xavi Hernandez alisema kwa kiasi fulani ni kama yanapotosha ukweli na hivyo amewataka yasiwafanye wachezaji wake wajiamini kwa sana.
“Kwa kiasi fulani matokeo ni kama yanapotosha, hatutakiwi kuwa wenye kujiamini kwa sana, ni matokeo mazuri kwetu lakini hayana maana kwamba tulicheza kwa kiwango bora sana,” alisema Xavi.
Alifafanua zaidi kwa kusema kwamba ni aina ya mechi ambayo ina mambo yaliyokuwa sawa kwa timu zote kwani Madrid nao walitengeneza nafasi nyingi wao (Barca) wana mambo mengi ya kufanya kuboresha timu yao.
Matokeo hayo ni mwendelezo wa mechi nyingine za kirafiki zilizochezwa hapo kabla ambapo, Man United ililala kwa mabao 2-0 mbele ya Real Madrid wakati Arsenal nayo iliichapa Barca mabao 5-3.
Kwa upande wake kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema matokeo ya mechi hiyo si muhimu sana na ingawa inaumiza kufungwa lakini wataendelea na mambo mazuri waliyoyafanya huko nyuma na kuisifu timu yake kwa kutengeneza nafasi nyingi.
Barca watakamilisha ziara hiyo ya mechi za kirafiki Jumanne hii kwa kucheza na AC Milan mjini Lass Vegas wakati siku inayofuata Real Madrid wao watakabiliana na Juventus mjini Orlando.
Kimataifa Barca yaichapa Real Madrid 3-0
Barca yaichapa Real Madrid 3-0
Read also
