Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba SC, Juma Mgunda amekuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la Vijana na timu ya Wanawake.
Hayo yameelezwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula akifafanua kuwa kocha huyo pia mbali na wadhifa huo, atakuwa na programu maalum kwenye maeneo ya timu za vijana, wanawake na timu ya wakubwa kwa ajili ya kuisambaza falsafa ya Simba.
“Niwaambie kuwa mwalimu Mgunda sasa hivi tunamtumia kwa programu maalum, kwa hiyo mtamuona kwenye maeneo mengi ya timu. Tutamtumia kama mwalimu ambaye anazunguka kwenye timu zote za vijana, Simba Queens na timu ya wakubwa.
“Klabu yoyote kubwa huwa na mwalimu ambaye anafanya kazi zaidi ya moja kwa sababu lazima zile falsafa za timu zianzie kwenye timu za vijana hadi timu ya wakubwa lakini hata timu ya wanawake,” alisema Kajula.
Licha ya Mgunda kupewa wadhifa huo lakini bado mpaka sasa pengo la nafasi yake ya kocha msaidizi halijapatiwa mrithi, ikielezwa muda si mrefu uongozi wa Simba utaweka wazi.
Mgunda alijiunga Simba Septemba, mwaka jana kama kocha wa muda akitokea Coastal Union kurithi nafasi ya Mserbia, Zoran Maki kabla ya baadaye kuteuliwa kuwa kocha msaidizi baada ya kutua kwa Mbrazil, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ aliyekuwa akiinoa Vipers SC ya Uganda.
Soka Mgunda sasa mkurugenzi Simba
Mgunda sasa mkurugenzi Simba
Read also
