Auckland, New Zealand
Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia la Wanawake, Marekani leo Alhamisi wamelazimisha sare ya bao 1-1 na Uholanzi katika mechi ya Kundi E.
Uholanzi ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 17 lililofungwa na Jill Roord hali iliyoifanya Marekani kupambana hadi kusawazisha katika dakika ya 62 kwa bao lililofungwa na nahodha wa timu hiyo, Lindsey Horan.
Matokeo hayo yanakuwa pigo kwa Marekani ambayo katika mechi zake 13 zilizopita za michuano ya Kombe la Dunia haikupoteza hata mara moja na ni kama vile imenusurika kipigo kabla Horan hajaokoa jahazi.
Marekani hata hivyo inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne katika mechi zake mbili sawa na Uholanzi ambayo inashika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao baina ya timu hizo.
Katika mechi zijazo za kundi hilo zitakazochezwa Jumanne ijayo, Marekani itaumana na Ureno kwenye dimba la Eden Park mjini Auckland wakati Uholanzi itatoana jasho na Vietnam mjini Dunedin.
Matokeo mechi za Kombe la Dunia Wanawake…
Marekani 1-1 Uholanzi
Canada 2-1 Jamhuri ya Ireland
Japan 2-0 Costa Rica
Hispania 5-0 Zambia
Kombe la Dunia Marekani, Uholanzi zatoka sare
Marekani, Uholanzi zatoka sare
Read also
