Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe ameachwa katika kikosi cha timu hiyo kinachoelekea Japan kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2023-34 huku kukiwa na habari kwamba huenda asipate nafasi tena katika timu hiyo.
Mbappe mwenye miaka 24, katika siku za karibuni amekuwa mjadala kuhusu majaliwa yake PSG baada ya kukataa kusaini mkataba mpya licha ya mabosi wake kumtaka afanye hivyo au akubali kuuzwa.
Mshambuliaji huyo ana mwaka mmoja katika mkataba wake na mabosi PSG wana hofu ya kumuona akiondoka bila ya kupata chochote kama atakataa kusaini mkataba mpya sasa na kuondoka mwakani akiwa mchezaji huru.
Mbappe amewahi kutoa msimamo wake akisema kwamba hataki kuondoka PSG kwa wakati huu lakini hayuko tayari kusaini mkataba mpya jambo ambalo limeibua utata kati yake na mabosi wa PSG .
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi aliweka wazi suala hilo wiki kadhaa zilizopita akisema Mbappe lazima asaini mkataba mpya kama anataka kuendelea kubaki na timu hiyo.
“Wachezaji ambao hawataki kubaki hapa, mlango upo wazi,” alisema Al-Khelaifi katika kauli yake nyingine ya hivi majuzi bila ya kutaja jina ingawa mlengwa mkuu wa kauli hiyo anaweza kuwa ni Mbappe, mfungaji bora wa Ligi 1 katika misimu mitano iliyopita.
Kinachoonekana sasa ni kwamba mabosi PSG wakiongozwa na Al-Khelaifi wameamua kuchukua uamuzi mgumu na Mbappe anadaiwa kuwa tayari kwa uamuzi huo.
Ikitokea Mbappe akabaki PSG hadi mwakani, itakuwa hasara kwa PSG kwa kuwa haitopata chochote kwa mchezaji huyo iliyemnunua mwaka 2017 kutoka klabu ya Monaco kwa ada ya Dola 197 milioni.
Mbappe ambaye pia ni mshambuliaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Ufaransa, jana Ijumaa alicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Le Harve na kufunga bao wakati PSG ikitoka na ushindi wa mabao 2-0, anawaniwa na Real Madrid ambayo inafuatilia kwa karibu kina
