Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva amesema anatarajia kutua kwenye timu za nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kulingana na ofa anazopokea kutoka huko.
Msuva aliyemaliza mkataba wake na klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia yuko huru kwa sasa akisema licha ya kupata pia ofa nyingine kutoka timu za Afrika lakini jicho lake lipo Uarabuni kutokana na maslahi anayotarajia kuyapata.
“Sina hakika kama nitarudi (Qadsiah) na sijafanya maamuzi nakwenda wapi na sina presha yoyote, kama niliweza kukaa miezi sita kabla sina timu na nikapata timu kwa nini niwe na presha sasa wakati nimecheza na nimemaliza na goli na ‘asisti’ moja.
“Sihitaji kuongea sana lakini mimi nipo huru, popote nitakapojaaliwa basi Mungu ndio amependa, ofa zinakuja nyingi tofauti tofauti za Afrika na UAE, yaani Asia na mimi mpango wangu mkubwa ni Asia, ikitokea Ulaya sawa lakini inategemea na kiasi ambacho kitakuwepo,” alisema Msuva.
Msuva alifafanua kuwa hategemei sana kwenda Ulaya kutokana na umri wa miaka 29 alionao, akisema anachoangalia sasa ni kuingiza pesa tu na si kushinda tuzo ya Ballon d’Or au medali za makombe.
“Ulaya sijaweka asilimia 100, nimeweka sana Asia na Afrika sababu Ulaya wanaangalia sana umri, kwa hiyo lazima niangalie fedha, siwezi tena kuanza kufikiria kingine, sihitaji Ballon d’Or wala medali, ndio maana hata medali yangu kule Wydad (AC ya Morocco) niliiacha,” alieleza Msuva.
Kimataifa Msuva apiga hesabu za Arabuni
Msuva apiga hesabu za Arabuni
Read also
